Status Auto Post

Panga status zako za WhatsApp (maandishi, picha, video) — zinapostiwa zenyewe kwa wakati uliochagua.

Toleo 1.0.0 · 3.9 MB · Android 10 au zaidi

Pakua APK

Toleo la kwanza: panga status za WhatsApp, kalenda, Kiswahili/English, trial na vifurushi.

Ukifungua akaunti unapata trial ya bure: saa 24 au status 5.

Jinsi ya kusakinisha

  1. Gusa Pakua APK. Ikimaliza, fungua faili StatusAutoPost-…apk (kwenye arifa au Files → Downloads).
  2. Simu ikisema imezuia programu kutoka chanzo hiki: gusa Settings, washa Allow from this source, rudi, gusa Install.
  3. Google Play Protect ikionya: gusa More details → Install anyway (inatokea kwa sababu app haitoki Play Store).
  4. Fungua app, Fungua akaunti, kisha fuata mwongozo wa mwanzo.
  5. Kwenye hatua ya Accessibility: chagua Status Auto Post na uiwashe.
    Android 13 au zaidi: swichi ikiwa imefifia ("Restricted setting"), fungua Settings → Apps → Status Auto Post → ⋮ (juu kulia) → Allow restricted settings, kisha urudi kuiwasha.
  6. Ruhusu kengele sahihi, arifa, na betri bila kizuizi. Kwa Tecno / Infinix / itel / Xiaomi fuata maelekezo ya simu yako yaliyo ndani ya app.
  7. Post status moja kwa mkono kwenye WhatsApp mara ya kwanza, kisha tuma status ya majaribio kwenye app.

Kama ulikuwa na toleo la majaribio (PoC) la zamani na usakinishaji ukakataa ("App not installed"), futa toleo la zamani kwanza, kisha sakinisha hili.

Taarifa muhimu: App hii hutumia WhatsApp yako rasmi kupost status ulizopanga wewe. Hatuwezi kuahidi kwamba akaunti yako ya WhatsApp haitazuiliwa — WhatsApp ina sheria zake. Tumia kwa kiasi, post maudhui yako mwenyewe, na usitumie kwa spam.